KILIMO NI AJIRA KUBWA KWA VIJANA
Vijana wengi wamekua wakiona kilimo ni cha watu wa makundi fulani au adhabu bila kujua kilimo kikichukuliwa kama ajira kinalipa. Balton Tanzania kwa muda mrefu imejikita katika kutoa elimu na usambazaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima wadogo wadogo wakiwemo vijana na kuwaelekeza kulima kwa malengo ya kibiashara. Alipokuwa anazindua kampeni ya Kilimo ni bomba Tanzania au Farming is cool Tanzania, mh. Dr. Bilal makamu wa raisi wa Tanzania awamu ya nne, aliwasisitizia vijana kujiajiri kwa kutumia aridhi ambayo Tanzania imejaliwa kwenye kilimo. Angiongelea kwa upande wa teknolojia alibainisha kwamba, imekua kwa kiasi kikubwa na pembejeo za kilimo zimerahisishwa kulinganisha na miaka iliyopita. Kwa kutumia mfumo wa umwagiliaji, mbolea na mbegu za kisasa, madawa n.k unauwezo wa kulima sehemu ndogo na kuvuma mazao mengi yanayoweza kukidhi mahitaji ya nymbani na mengine kuuza.