Binti wa miaka 5 atoa elimu ya kilimo

Ni katika shamba la mzee Valentino Nanyaro, nakutana na  watoto watatu wa familia moja.

Wamezungukwa na kundi kubwa la watu wakiangalia ustadi wao wa kumudu kutumia mbinu mbalimbali za kilimo cha kisasa zinazosambazwa na kufundishwa na kampuni ya Balton Tanzania inayojishughulisha na usambazaji na mafunzo ya pembejeo za kilimo.

Ni ajabu iliyoje! Ni watoto wadogo wenye umri kati ya mika 5 hadi 13 wakionyesha na kueleza mbinu za kilimo cha kisasa kama  zinavyofundishwa na kuelekezwa na wataalamu wa kilimo.

Mtoto mmoja kati ya hao watatu ananikaribisha kwa tabasamu la mbali, huku  mkononi mwake akiwa ameshika nyenzo ya kutengenezea mashimo madogo ya miche ya mbogamboga.

“Njoo uone” ananikaribisha kwa tabasamu angavu. Hapa nalazimika kumuuliza jina lake… “Naitwa Eva” ananitajia jina kwa sauti ya hofu huku akinipa mgongo na kuelekea katika kitalu chake. 

Ninapomuuliza Eva (5) ni jinsi gani amejifunza kupanda vitunguu, nashikwa na butwaa kwa maelezo yake yake yaliyojaa utaalamu mwingi.

 “Kwanza lazima uandae matuta kama hivi”…(anaonyesha), kisha Balton wanakuja kukuwekea mipira ya kumwagilia mazao”.

Kifupi, hatua za kilimo ambazo wakulima hufundishwa, Eva anazitaja kuwa ni uandaaji wa  shamba, uwekaji wa mipira ya umwagiliaji kwa njia ya matone na utengenezaji wa mashimo yenye hatua sahihi kwa ajili ya upandaji wa miche na kuweka mbolea ya awali.

Mbali na Eva, shambani hapo yupo mtoto mwingine. Huyu anaitwa Philemon Valentino na ni kaka wa Eva.

Akiwa na miaka 13 tayari ameshakuwa mjuzi wa kilimo cha mboga kinachotumia miundombinu ya kisasa. Anasema kuwa utaalamu huo kaupokea kutoka kwa baba yake

“Wataalamu wa Balton wanapokuja kumtembelea baba shambani na kumuelekeza masuala ya kilimo nasi pia huwa tunakaa pembeni na kusikiliza ili kujifunza, na ndio maana unaona tunafanya wenyewe hapa na baba anatuamini. Shughuli hizi huwa tunafanya siku ambazo hatuendi shuleni”anasema.

“Mimi ni mkulima wa siku nyingi na nilipendezwa na hii teknolojia inayosambazwa na watu wa Balton baada ya kuona kilimo nilichokua nafanya ni cha kizamani na hakina tija. Mazao niliyoyapata yalikua kidogo na hafifu kabla ya kuingia kwenye mfumo wa umwagiliaji. Baada ya kuona ni faida kwangu nilitaka watoto wangu nao wajifunze kilimo kwani ndio ajira za kesho. Zamani tulifundishwa kilimo mashuleni japo kilikua kigumu ukilinganisha na cha kisasa ila, kilimetufunza mengi moja wapo ni kujitegemea, hata kama ningefeli shuleni bado ningekua na uwezo wa kujitegemea. Watoto wengi wa siku hizi wanategemea wazazi kwa kila kitu hata kusumbua akili hawataki. Ni misingi mibovu tunayowajengea na sio kuwapa mwelekeo bora, mwisho wa siku wanategeneza makundi ya tabia mbaya mfano; wizi, ulevi, uzaaji wa madawa ya kulevya n.k” Anasema mzee Valentino.

Nilipomuuliza nini wito wako kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuhusu kilimo na kizazi kijacho? alisema “ Samaki mkunje akingali mbichi” ninamaanisha watoto wafundishwe kilimo cha kisasa wakingali wadogo kwani zamani tulikua tunafanya kilimo duni na cha mazoea na tulikufa masikini. Siku hizi unaweza ukalima eneo dogo ila mazao ya kutosheleza kula na biashara.” Alimalizia mzee Valentino kwa msisitizo na tabasamu laini.

Ukiweza kumpata mzee valentine muulize nini kilimsukumua kuwafunza watoto wake kilimo, anajisikiaje watoto wale kuwa wajuzi wa kilimo, ana wito gani kwa wazazi na jamii kwa jumla

Safari ya Arusha katika shamba la Mzee Valentino linatufundisha haja ya wazazi kuwafundisha watoto wao mbinu za kilimo cha kisasa kwa manufaa yao, jamii na Taifa kwa jumla.

Aidha, haya ni mafunzo yanayopaswa kutolewa kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali za elimu nchini, ili yawe chachu ya kujiajiri kwenye sekta ya kilimo.

Balton kupitia kampeni yake ya "farming is cool Tanzania" au "kilimo bomba" inayomlenga zaidi kijana, imejipanga kutoa elimu hii ya kilimo cha kisasa kwenye shule zaidi ya 200 nchini.

Shule hizi zinatakiwa kuwa na vigezo ambavyo Balton itavitoa mara baada ya mipango ya awali ya kampeni hii kukamilika.

“Endapo elimu hii ya kilimo cha kisasa itatolewa katisha shule za msingi hadi vyuo vikuu, kutakuwa na ongezeko kubwa la vijana kujiajiri kwenye sekta ya kilimo,’’ anasema Ofisa uhusiano wa Balton, Linda Byaba.

Imeandaliwa na: Linda Byaba